LONDON, ENGLAND
HABARI kutoka England zinasema kocha wa Manchester United, Alex Ferguson ataachana na soka mapema mwakani.
Kocha huyo raia wa Scotland ambaye alitimiza miaka 26 kwenye klabu
hiyo na kupewa heshima ya mnara wikiendi iliyopita, amefikisha miaka 70
na anaona kwamba ni wakati mwafaka wa kupumzika.
Imekuwa ni kawaida kwa Ferguson kusema kuwa ataachana na soka
karibuni lakini habari kutoka katika familia yake zinasema kuwa kocha
huyo sasa anataka kuachana na mchezo huo mwakani na kama ikiwezekana
baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu England.
Kocha huyo ambaye ameipatia klabu yake vikombe 19 vya Ligi Kuu
anatimiza miaka 71 mwezi ujao na anadhani ameshawatumikia wapenzi wa
klabu vya kutosha.
Kumekuwa na tetesi kuwa iwapo kocha Alex atastaafu nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Jose Mourinho au Pep Guardiola.
No comments:
Post a Comment