THERE IS NO NEED TO DREAM IN NATURE BECAUSE YOU ARE ALREADY INSIDE THE DREAM.
Thursday, December 13, 2012
KAULI YA CHADEMA KUHUSU MAGUFULI KUMPIGIA DEBE ODINGA KENYA
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia CHADEMA kimeitaka Serikali kutolea ufafanuzi suala la WazirI wa ujenzi Dr. John Magufulu kuhudhuria Sherehe za kutambulishwa kwa mgombea urais chama cha ODM Kenya Raila Odinga endapo suala hilo lina uhusiano wowote wa Kiserikali.
Mkurugenzi wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Ezekiel Wenje(pichani kushoto) amesema kitendo cha waziri huyo kuhudhuria sherehe za kutambulishwa wa Raila kinatoa picha mbaya ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya iliyopo Madarakani kutokana na ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali hizo.
kwenye sentensi nyingine Wenje amesema Magufuli kupanda jukwaani kuanza kumnadi kiongozi wa ODM ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kimataifa ambapo amedai kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa mataifa ni kosa kubwa Taifa moja kuingilia siasa za Taifa jingine hata kama hayo mataifa yanaushirikiano wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment